NEWTONE (The hip hop Icon)

Newtone ni msanii wa miondoko ya Hip Hop ambaye anaishi jijini Dar-es-Salaam. Historia yake ya Muziki inarudi miaka nane nyuma (2003) ambapo ndipo alipoanza jihusisha na masuala ya Muziki huu wa hip hop. Akiwa kidato cha kwanza alianza tabia ya kuandika mistari ya hip hop kiasi ambacho watu wengi walimkubali na kuona kuwa uwezo wake pengine utaweza wasumbua wakongwe wa enzi hizo ambao walikuwa wakisumbua kama akina Professa Jay, fid Q na wengine. Ilipofika mwaka 2005 alibahatika kuingia studio kwa mara ya kwanza na kufanya nyimbo yake ya kwanza ambapo kutokana na kujihusisha na masomo alishindwa kushikilia vitu viwili kwa mpigo na badala yake akaamua kuendelea na masomo kwanza. Alipomaliza kidato cha sita mnamo mwaka 2009, NEWTONE alifanikiwa kurekodi ngoma nyingine iliyokwenda kwa jina la “Sayari Yetu” aliyoifanya star wa miondoko ya RnB Tanzania anayeitwa BELLE 9. Ngoma hiyo ambayo iliweza pigwa katika baadhi ya Radio Station na kupata kumtambulisha kwa kiasi fulani katika tasnia hii ya muziki wa hihop nchini. 

Akiwa amejiunga na chuo cha Science kinachoitwa Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) Newtone akaachia ngoma nyingine ambayo aliifanya katika Studio za DIRTY MODE RECORDS chini ya Producer Triple akimshirikisha msanii wa Studio hiyo anayekwenda kwa jina la STONE, ngoma ikienda kwa jina la “TIME”. Ngoma hii ilifanya vizuri katika baadhi ya vituo vya Radio vya mikoani ikiwa na Mwanza, Dar-es-salaam, Morogoro, Arusha na mingineyo. Ku DOWNLOAD ngoma ya "TIME", tembelea ukurasa wa Downloads kwenye blog hii ili uweze kuipata ngoma hiyo..
Baadaye mwaka huu, Newtone amerudi na Track nyingine akiwa kwenye kundi akishirikiana na Msanii mwenzake anayeitwa SICSO B Ngoma ikiwa inaenda kwa jina la HOLD ME TIGHT wakimshirikisha Producer ambaye ndiye aliyehusika na kufanyika kwa ngoma hiyo anaitwa TRISS. Ngoma ilyo katika “Tachez” za kimodern na ambayo tayari imeshaanza kuenea kwa kasi katika sehemu mbali mbali za nchi kupitia Internet na radio Stations. Ngoma hii unaweza kui- DOWNLOAD kwenye link hiyo hapo chini. 
Ukiachilia mbali track hizo. Newtone ameshiriki katika collabo ambayo inafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio, track hii inaitwa ALAMA ZA NYAKATI. Vile vile jamaa huyu anajihusisha na masuala ya VIDEO PRODUCTION na SOON tutamsikia humu kuhusu ndoto na kazi zake.

0 comments:

Post a Comment