New Kid anaekwenda kwa jina la TiNTO amekuja na nyimbo ambayo kwa haraka tunaweza sema ndio inamtambulisha rasmi kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya a.k.a bongo flava.

Maadhi na mtindo wake wa kutembea na beats ni wa kipekee kabisa kulingnishwa na wasanii wengine ambao tunawasikia. Sikiliza wimbo wake huu kupitia hapa. Soon atakuja na nyimbo kubwa zaidi akiwa anazidi onyesha uwezo wake. 


LYRICS: NIPO LIKIZO+MP3 DOWNLOAD.

NEWTONE FT NEYAH & BELLE 9

CHORUS
NEYAH-Ni zaidi ya pigo kuhisi ulimwengu wako siwangu tena,
BELLE 9-lile jalada la stress me nishalifunga staki me,
NEYAH-kukupenda wewe mzigo mzito sinabudi kuweka kando,
BELLE 9-nipo likizo kwa sasa me nipo likizo utanisamehe.

VERSE 1
Ulinipa mawazo ikanishangaza hadi vikwazo,
viliibuka nikashtuka na nikajua nini chanzo,
uliniteka kwa hisia ukanicheka nikilia,
kwangu ulideka na ukasepa sina mkwanja nikaumia,
spigi pamba najua, ilichangia ukanitenda ukanitenga
hadi miradi yangu yote ukaichukua ,for the bitch u av
become lady, i never ever wanna see you,
huu ndo muda wakuongeza bidii tu,yeah mapenzi nipo likizo,
yanachosha mapenzi ya ushenzi na matatizo,
yakianza unapumbazwa yanashamiri kwa furaha,
yakiisha yanatisha huwezi himili ni karaha,
nyumbani hukupenda kaa, super star wa mitaa,
na kidogo nilichokupa ulikwenda shindia bar,
ubongo upate tulizo nisihishi kwa viulizo,
kwenye moto wa mahaba wenye raha na vikwazo,

CHORUS
NEYAH-Ni zaidi ya pigo kuhisi ulimwengu wako siwangu tena,
BELLE 9-lile jalada la stress me nishalifunga staki me,
NEYAH-kukupenda wewe mzigo mzito sinabudi kuweka kando,
BELLE 9-nipo likizo kwa sasa me nipo likizo utanisamehe.

VERSE 2
Ambapo hakuna suluhisho ni dhairi hakuna tatizo,
mapenzi kweli yanatesa ndomana nipo likizo,
nimechoshwa na mizozo,kukicha haiishi
silambi tena matapishi kuishi kama vile warzone,
woriz born sio tanga, maulana ndo kayaumba huu ni
ugonjwa na pia huwezi jiganga, najipanga!
haya maisha nisije disco,
sababu sap ya mapenzi ilinifanya me ni lose hope,
yeah ridhiki mafungu kumi, toa saba ya roho ya paka huku
data na mtoto wa kihuni,mtoto ukambemenda wala hukumjali,
toa penzi unapewa pesa unasepa haukuona hatari,
kwa sasa staki stress nipo against,
hasira na wivu sihitaji shari tangu nimekufuma guest,
mwili vuguvugu huku penzi motomoto ndo ukanifanya minidate
toka enzi za fungate,na sali, namuomba mungu huku mishe anazibless,
haba haba full kibaba bado maisha naya set,
mwisho wa likizo sijaujua nashukuru,
ilhali minapumua matatizo yanapungua,

CHORUS
NEYAH-Ni zaidi ya pigo kuhisi ulimwengu wako siwangu tena
BELLE 9-lile jalada la stress me nishalifunga staki me
NEYAH-kukupenda wewe mzigo mzito sinabudi kuweka kando
BELLE 9-nipo likizo kwa sasa me nipo likizo utanisamehe


New Joint inayokwenda kwa jina la "Nakupenda Sana" ya kwake Marley ndio ipo officially out. Ngoma Imefanyika na Producer Triss, Kama kawa ni Dirty Mode Records Recipes..

Awali Msanii huyu alikuja na Ngoma inayokwenda kwa jina la "Sina cha kupoteza" akimshirikisha Belle 9. 

Alipendwa sana kwa style yake ya Ragga kwenye Ngoma hiyo na ndipo wadau walipomshauri afanye kitu cha tofauti kidogo na hiphop kwa kuimba Sweet Raggae. 

Ngoma hii ni mfululizo wa ngoma nyingi zinazokuja za kijana huyu.

Keep Tuned kupitia hapahapa Dirty Mode Records Blog!!!!!.

DOWNLOAD NGOMA HII HAPA CHINI



DOWNLOAD SINA CHA KUPOTEZA Ft. Belle 9  HAPA


New talent kwa jina la Zero kutoka Mkoani morogoro. Ni masanii ambaye kwa kweli naweza sema ni wa pili kwa uwezo wa ki-RnB mkoani Morogoro ambaye anakuja kumuweka belle 9 katika wakati mgumu baada ya kuibuka na kufanya ngoma kali inayoitwa SIKUELEWI akimshirikisha Mr. Blue a.k.a Kabaisa.

Ngoma hii aliyofanya kwa kupitia studio za dirty Mode records chini ya Producer Triss, ndani ya week 1 tangu kuachiliwa rasmi (Officially released) tayari imeshaanza kufanya vizuri kupitia vituo mbali mbali vya radio vya Nchini Tanzania. 

Pia ukiachilia mbali Audio tayari msanii huyu ameshafanya bonge la VIDEO kwa Company ya Show Biz Defined chini ya Usimamizi wa director Mike Tee.

Unaweza kui-KUIDOWNLOAD ngoma hii kupitia hapa Chini…Soon Video link itakuwa hewani….


The brand New Video ya Marley ft. Belle 9 imeachiwa kwa njia ya internet na baadhi ya vituo vya television vya nchini Tanzania. 

Video hii imefanyika chini ya Company ya Video iitwayo Dirty Vision ambayo ipo affiliated na Dirty Mode Records. 

Video hii imefanyika kwa lengo la kuwafanya watanzania na fans wote wa Music wa Dirty Mode Records waweze kumfahamu Marley na kujua uwezo wake wa Music (Promo Only). 

Sikilizia ngoma hii ya msanii mwenye swags  za hip hop akichanganya na maadhi ya Raggae Dance Hall.

Soon jamaa huyu atakuja na Ngoma nyingine ambayo itafanyika chini ya studio hizihizi za Dirty mode Records. Enjoy the video na support.

1.Download Marley ft. Belle 9 Mp3 CLICK HERE
2.Follow Dirty Mode Records on Facebook CLICK HERE
3.Follow Dirty Mode Records on Twitter CLICK HERE