LAUNCHED CONTEST (WIN TZS 300, 000 RECORDING COUPON)



Shindano ambalo limesubiriwa kwa muda mrefu sasa lipo tayari. Dirty Mode Records imekuja na CONTEST/ SHINDANO lenye thamani ya TZS 300,000/= Recording Coupon (Kuponi ya Kurecord). Tunaposema Recording Coupon tunamaanisha kuwa Mshindi wa kwanza wa shindano hili atapata FURSA ya kuweza kufanya WIMBO MMOJA BURE katika STUDIO za Dirty Mode Records zilizopo Mjini Morogoro. Na si Lazima atayeshinda ndiye arekodi, bali anaweza Kuiuza kuponi hiyo au kuigawa kwa MTU YEYOTE ampendaye kwa makubaliano yao binafsi ambayo sisi HATUHUSIKI nayo.

Lengo la Mashindano haya ya HURU na WAZI ni kutoa nafasi kwa VIPAJI VIPYA kuweza pata nafasi ya kurekodi pasipo tumia gharama yoyote pia KUTOA ASANTE kwa wapenzi wa Dirty Mode kwa kuendelea kuthamini kazi zetu kwa kipindi chote cha Mwaka wa 2011

Tunapozungumzia Mashairi hatumaanishi yafuate taratibu zote za kiuandishi wa MASHAIRI bali yawe na LADHA na MVUTO ambayo wasanii wengine wa muziki nchini wanatumia ili kuburudisha na kuelimisha jamii (Haubanwi na kanuni). Ila kikubwa kinachotazamwa katika shindano hili ni kuandika mashairi yenye VINA.
Mashindano haya yataendeshwa katika FACEBOOK FAN PAGE ya Dirty Mode Records BONYEZA HAPA KUINGIA. Kwa hiyo ni jukumu lako kuandika mashairi MAZURI na yenye MVUTO ili kuwavutia watu ku-like pia kualika na kushawishi watu wengi kama rafiki zako walio FACEBOOK KUJOIN FANPAGE yetu ili waweze ku-LIKE shairi lako.

USHIRIKI:
Kila Mshiriki atatakiwa kufanya yafuatayo.
  1. MSHIRIKI anatakiwa ku-POST SHAIRI LAKE MOJA KWA MOJA Kwenye FACEBOOK FAN page yetu CLICK HAPA KUTEMBELEA PAGE YETU
    Unachotakiwa kufanya baada ya kutuma Shairi lako ni kuwahimiza Marafiki, Ndugu na jamaa zako walio FACEBOOK kulipigia kula kwa kuli "LIKE" Shairi lako ili liweze kupata Likes Nyingi kuliko mengine na mwisho uweze kuibuka mshindi.
    DONDOO:
  1. Mashairi yenye maadili na kusomwa na kila mtu, Na mtu YEYOTE RUKSA kushiriki
  2. Ushiriki wako utakuwa batili endapo utaenda kinyume na Utaratibu na vigezo vilivyowekwa. Na UTAFUTWA kwenye Page
  3. Hakikisha kiasi cha Mistari yako ni cha kiasi na kinaenea kwenye FACEBOOK post field,, ukizidisha maneno facebook page itagoma kutuma shairi lako.

    MAONI

    Kama una maoni juu ya Shindano hili tafadhari tutumie kwa Email yetu ya dirty_mode@yahoo.com. Ama kwa Contacts Page ya Blog yetu..
      

0 comments:

Post a Comment