DIRTY MODE RECORDS YAREKODI NA INTERNATIONAL ARTIST
Mwanamuziki wa Tanzania aishie nchini Sweden Jan B anatarajia kufanya ngoma na mwanamuziki wa kimataifa mwenye asili ya kilatin aishiye Sweden, Sayen.
Jan B amesema jana jioni alimaliza mazungumzo na Producer mmoja mkubwa wa kimataifa nchini humo kufanya ngoma yake inayoitwa ''YOU WAN IT''.
Cha kufurahisha zaidi ni kuwa beat ya wimbo huo imefanywa na producer aliyemtoa Belle 9 na ‘Sumu ya Penzi’, Tris, ambaye yupo Dirty Mode Records.
Amesema hata hivyo producer huyo wa kimataifa aitwaye Eduardo Moretti ataiboresha zaidi.
Kwenye chorus ya wimbo huo amesema Triss na SAYEN (kwenye Picha chini) watapokezana na huku kwenye bridge akisimama Sayen peke yake.
Amesema style ya wimbo huo itakuwa ni House/Pop na utakaokuwepo kwenye mixtape yake iitwayo ''Swahili swag''.
“Muda wowote kuanzia next week tunaingia studio kufanya kazi. Beat na vocal zote tayari Dirty mode records washakamilisha,” alisema Jan B.
SAYEN
PRODUCER TRISS (DIRTY MODE RECORDS)
0 comments:
Post a Comment