IZZO AZUNGUMZIA NGOMA YAKE MPYA "UTARUDISHWA"

Mwanamuziki mahili wa miondoko ya hip hop nchini maarufu kwa jina la Izzo Bizness kutoka mkoa wa Mbeya ametamka rasmi kupitia ukurasa wa facebook na kwa njia ya mawasiliano ya messeji na Dirty Mode Records kuwa kesho ya tarehe 31/07/2012 anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "UTARUDISHWA" ambapo humo ndani amemshirikisha msanii mkali wa RnB Belle 9. 

Ngoma hiyo inafuata baada ya kuachia video yake ya "Nakuchukia Mwaka Jana" na Imefanyika kwa kushirikiana na studio za Dirty Mode Records chini ya Produer mahili nchini Tanzania, Producer Triss. Izzo alisema kuwa ngoma hiyo ambayo anaamini itakuwa gumzo sana kwa watanzania kutokana na ilivyokuwa ya kitofauti itakuwa hewani kupitia vituo mbalimbali vya radio kuanzia kesho siku ya Jumanne.


"Watanzania Tunaomba Ushirikiano wenu wa dhati ku-support kazi hii pia kuona namna gani Dirty Mode inakubalika na kupewa nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa nchini na hata nje ya Nchi". 

Nyimbo hii itakuwa hewani kuanzia Kesho,, so usikiae mbali na radio yako pia kufikia kesho jioni ngoma hiyo itakuwa hapahapa kwa blog yako. Keep tuned...




0 comments:

Post a Comment