BIG DEAL KWA MSHINDI WA 2 & 3 NA WASHIRIKI WENGINE
Dirty Mode Records kupitia shindano la andika Lyrics imeamua kutoa complementary kwa mshindi wa PILI na wa TATU wa shindano hili ambalo linatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa tano (MAY). Hatua hii imechukuliwa baada ya kupata maoni kutoka kwa washiriki wengi na wadau wengine ambao wanaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa mtu ambaye atakuwa amebahatika kuwa mtu wa pili ama wa tatu.
AINA YA ZAWADI KWA MSHINDI WA PILI:
Mshindi wa PILI wa shindano hili atapewa nafasi ya kurekodi katika studio za dirty mode records kwa kupata kuponi ya punguzo la 60% za kulipia wimbo wake mmoja hivyo kutakiwa kulipia TZS 120, 000 tu. Punguzo hili litadumu kwa kipindi cha siku 30 baada ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hili.
AINA YA ZAWADI KWA MSHINDI WA TATU:
Mshindi wa TATU wa shindano hili atapewa nafasi ya kurekodi katika studio za dirty mode records kwa kupata kuponi ya punguzo la 50% za kulipia wimbo wake mmoja hivyo kutakiwa kulipia TZS 150, 000 tu. Punguzo hili litadumu kwa kipindi cha siku 30 baada ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hili.
KWA WASHIRIKI WOTE:
Kwa wale walioshiriki na wanadhani wao wanaweza kufanya vizuri endapo wangepewa nafasi ya kurekodi na studio yetu tutawatangazia utaratibu wa kuweza kuwasiliana na sisi kupata kuwasikia na kujua tunawezaje kuwasidia kufikia malengo yenu. Endapo kati yenu kuna mtu mwenye uwezo wa kuishwishi menejimenti ya studio kumchagua kurekodi yatafanyika hivyo. Its a BIG DEAL mazeee...Kazeni na mchakalikie maisha hayoooo.... TUNAWAPENDA WOTE....
ANGALIZO:
Washiriki mnahimizwa kuendelea kufanya hima kushiriki katika shindano hili bila kukata tamaa kwani msimu wa zawadi kwa mashabiki wa Dirty Mode Records umepania kuweza kuwapa mashabiki wake mambo mazuri na yenye kuleta maslahi kwa wasanii na wapenda mziki wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment