EAST AFRICA RADIO DJ ATOA SUPPORT KWA CONTEST

"Niaje mazee Call me DJ SUMMER napatikana pande za EAST AFRICA RADIO/TV kipindi cha POWER JAMS (Jumatano) na CRUISE (Ijumaa). kwanza kabisa napenda kuwapongeza wote ambao mnaonesha ushirikiano wenu ata kwa kusoma tu maandishi haya kwani ni mchango mkubwa sana".

Nafurahishwa sana ninapoona vijana tunashirikiana kwa kujiendeleza muziki wa hapa nyumbani (bongo fleva) sisi wenyewe kwani huo ndio ushirikiano ambao tunatakiwa kua nao vijana wa kitanzania na tusisubiri mtu wa nje ndio aje kutusaidia.


kikubwa kilichonivutia hadi nikajikuta na mimi nahitaji kuwa mmoja wapo kati ya watu wanaoweza kuwa msaada pia, ni shindano la kuandika mistari ya hip hop ambalo limeandaliwa na studio ya muziki inayofahanika kama DIRTY MODE RECORDS ambayo inapatikana pande za morogoro na kumfanya mshindi apate nafasi ya kurekodi nyimbo yake bure kabisa hivi ndivo vijana wa kitanzania tunatakiwa kuwa kwani mwisho wa siku tunapofanya vizuri sifa inakuja kwa watanzania ambao ndio sisi.

Na mimi kama DJ ambaye nafanya ngoma za tanzania zinavuka boda na kusikika africa mashariki kupitia East Africa Radio niko tayari kwa kuwapa mchango wangu wasanii wote ambao wanachipukia na hata ambao tayari wana majina makubwa so kama una ngoma yako ambayo tayari imesha rekodiwa fanya kuitupia hapa music@eastafricaradio.com na moja kwa moja itatufikia na tukiona iko poa itapata nafasi ya kusikilizwa africa mashariki bila shaka.

Na kwa wale ambao wanakipaji na hawana uwezo wa kwenda studio shindano ndo hilo hapo liko hewani kwani DIRTY MODE RECORDS wameona kwamba wanaweza kuwa msaada kwako so fanya kutupia mashahiri ya ukweli na mwisho wa siku utajikuta unang'aa kama mastaa wengine wa muziki wa bongo na hata nje pia.


mimi sina la zaidi nawapongeza sana DIRTY MODE RECORDS na wote waliohusika na kuandaa shindano hili safi sana kwani ni changamoto kwa vijana wa kitanzania...

kwa wale wanaoitaji kusomana na mimi kwa lolote lile.

facebook.

[dxj ssummer tze]

twitter.

[@dxjsummer]

na zaidi sikilia EAST AFRICA RADIO na kuangalia EAST AFRICA TV your all hits station.

1 comments:

Shukrani sana mkuu kwa kutupa mistari ya ukweli ngoja tugonge kazi sasa ili upaze sauti zetu hewani.

May 17, 2012 at 3:42 AM comment-delete

Post a Comment