WASHINDI WA LYRICS CONTEST 2011

Kufuatia kinyan'ganyiro cha kumtafuta mshindi wa shindano la andika mashairi kupitia studio Mashuhuri Morogoro na Tanzania kwa ujumla kutokana na kufanya kazi na wasanii wakubwa na kuweka baadhi ya nyimbo kali katika nafasi kama ya Belle 9 Amerudi wa wengne wengi , Dirty Mode Records. Hatimaye kilele chake kilifikia jana usiku ambapo washindi watatu walienda kupatikana. Kama ilivyonukuliwa kutoka kwenye page yetu ya Facebook BONYEZA HAPA KUTEMBELEA .


Mshindi wa KWANZA ambaye ni MANGALA WA AISHA (kwenye picha pembeni) kutoka pande za Dar- Es- Salaam, ameibuka na kinyan'ganyiro hicho kwa kuwa na kura zipatazo 192.

Mshindi wa PILI ambaye anaitwa STEVIE OKEYO STEJOH kutoka pande za Arusha, ameibuka na kuwa na kura zipatazo 81 akiwa ameachwa kwa tofauti ya kura 111 kutoka kwa mshindi wa kwanza.

Mshindi wa TATU ambaye anaitwa DRAVIC MOUDY kutoka pande za Dar- Es- Salaam, ameibuka na kuwa na kura zipatazo 73 akiwa ameachwa kwa tofauti ya kura 8 kutoka kwa mshindi wa pili. Jitihada kidogo zilihitajika kumfikia huyu jamaa.

NAMNA YA KUPATA ZAWADI:
Mshindi wa KWANZA atatakiwa kuja Morogoro ambapo studio zetu zilipo ili kuweza kuifanya nyimbo hiyo BUREEE kabisa kuanzia uandaaji wa mwanzo mpaka mwisho. Tarehe na siku ya zoezi hilo lipo kwenye mchakato kwani mawasiliano ya mtu huyu yameshapatikana ili kuweza kujua zoezi hilo linaisha katika taratibu zipi.

Mshindi wa PILI na wa TATU watatakiwa kufanya yafuatayo kama taratibu za awali zilivyotangazwa.

Mshindi wa PILI wa shindano hili mejinyakulia nafasi ya kurekodi katika studio za dirty mode records kwa kupata kuponi ya punguzo la  60% za kulipia wimbo wake mmoja hivyo kutakiwa kulipia TZS 120, 000 tu. Punguzo hili litadumu kwa kipindi cha siku 30 baada ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hili. Mawasiliano ya awali yameshafanyika ili kuweza kujua tunamaliza vipi zoezi hili kwa ushirikiano kama tulivyoahidi


Mshindi wa TATU wa shindano hili amejinyakulia nafasi ya kurekodi katika studio za dirty mode records kwa kupata kuponi ya punguzo la  50% za kulipia wimbo wake mmoja hivyo kutakiwa kulipia TZS 150, 000 tu. Punguzo hili litadumu kwa kipindi cha siku 30 baada ya kutangazwa kwa mshindi wa shindano hili. Mawasiliano ya awali yameshafanyika ili kuweza kujua tunamaliza vipi zoezi hili kwa ushirikiano kama tulivyoahidi.

Uongozi wa Dirty Mode Records unatoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki kulifanikisha hasa kwa watu wote walioonyesha moyo wao  kushirikiri katika kuwapigia kura washiriki wote. Kwa haya machache tunasema Ahsanteni sana na endeleeni kufuatilia kazi za dirty Mode kwani mambo mengi mazuri yanakuja njiani.  One love....



0 comments:

Post a Comment