DJ CHOKA AONGEA NENO

DJ maarufu nchini Tanzania, DJ CHOKA a.k. a Mr. Appetite leo amefunguka kupitia Facebook maneno ambayo kwa kweli makampuni ya media na vyombo vya burudani Tanzania wanapaswa kujifunza ili muziki wetu wa Bongo uzidi kwenda juuu na wadau wa muzii huu wanafaike zaidi.

Jamaa amesema kama ifuatwavyo na nukuu: 

"Nilipokuwa South Africa nilijifunza vitu vingi sana haswa kwenye maswala ya muziki na media kwa ujumla. Wale jamaa kuanzia radio, tv hadi clubs zao wanapiga mziki wao sana kuliko mziki unaotoka nje ya nchi yao. Sasa mimi nadhani mziki wetu bongo ukipewa nafasi ya asilimia 90 halafu 10 zikiwa ni mziki kutoka nje ya nchi yetu nadhani wasanii wetu watafika mbali hata kwa kipato tu watakuwa juu, mfano upo wazi kwa baadhi ya wasanii wetu wakongwe ambao walivuma zamani lakini angali maisha anayoishi sasa hivi hayaendani na mziki waliokuwa wakiuimba hapo nyuma. 

TUPENDE KUSIKILIZA VITU VYA NYUMBANI KWANZA HALAFU BAADAE TUSIKILIZEA MZIKI WA NJE KWA KUJIFUNZA ZAIDI"


Download New Music @ CLICK HERE NEW DIRTY MODE MUSICS DOWNLOADS MP3
Follow Us on Facebook @ CLICK HERE PLEASE
Follow Us on TwitterCLICK HERE PLEASE

0 comments:

Post a Comment